Nafasi Za Kuwa Mjumbe Wa Kamati Za Mikoa Za Watumiaji Wa – Dar es salaam – SUMATRA Consumer Counsultative Council

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA Consumer Counsultative Council) limeanzishwa chini ya kifungu namba 29 cha Sheria ya SUMATRA, Namba 09 ya mwaka 2001. Moja ya majukumu yake ni pamoja kuanzisha kamati za mikoa za watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini.
Hivyo basi, Baraza linatangaza nafasi za kuwa mjumbe wa Kamati za Mikoa za Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Arusha, Mtwara, Tanga, Kigoma na Mbeya.

MAJUKUMU YA WAJUMBE WA KAMATI ZA WATUMIAJI.
i. Kuelimisha watumiaji wa huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini juu Haki na Wajibu wao.
ii. Kuratibu kazi na maendeleo ya Vilabu vya Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
iii. Kufuatilia hali halisi ya usafiri ndani ya mkoa husika na kutoa taarifa kwa Katibu Mtendaji wa Baraza.
iv. Kushirikiana na Mamlaka ya SUMATRA katika mkoa husika, serikali ya mkoa na halmashauri zake juu ya namna bora ya kuboresha huduma za usafiri kwa kuzingatia Haki na maslahi ya Mtumiaji wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini.
v. Kuwa kiungo baina ya watumiaji,serikali katika mkoa husika na Baraza.
vi. Kusambaza taarifa na maoni ya watumiaji kwa mamlaka ya SUMATRA mkoani na wadau wengine.
vii. Atafanya majukumu mengine atakayoelekezwa na Katibu Mtendaji au watakayo kubaliana kwenye kamati ya mkoa ya Watumiaji kulingana na uhitaji wa mazingira na wakati husika.

MASLAHI YA WAJUMBE.
• Hakuna ujira.Kazi za Kamati za mkoa za watumiaji zitafanywa kwa kujitolea.

SIFA ZA MWOMBAJI.
i. Asiwe mmiliki wa chombo chochote cha kutoa huduma ya usafiri wa nchi kavu na Majini.
ii. Awe anaishi au ni mwajiriwa ndani ya mkoa husika (atakaoomba).
iii. Awe Mtanzania,mwenye akili timamu, mchapa kazi na mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea .
iv. Awe mwenye nguvu, moyo na nafasi ya kujitolea kufanya kazi na kujituma kwa ajili ya kuisaidia jamii juu ya masuala yanayohusu usafiri.
v. Awe anajua kusoma na kuandika lugha ya Kiswahili na uwezo wa kuwasiliana na watu
vi. Awe mzalendo na mwaminifu kwa mali na rasimali za Umma.

Mtu yeyote mwenye sifa hizo hapo juu atume maombi kwa anuani au barua pepe ya Baraza, ukiambatanisha Wasifu wako (CV), Vivuli vya Vyeti vya Elimu, ndani ya siku 21 tangu tarehe ya kwanza yaTangazo hili kutoka.
Katibu Mtendaji,
Baraza la Ushauri la SUMATRA, Jengo la NSSF Waterfront ghorofa ya 7,
S.L.P.14154,
Dar es salaam.
Barua pepe info@sumatraccc.go.tz
NB: Tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya Baraza: www.sumatraccc.go.tz

[yuzo_related]